Baada ya kufanya kazi kubwa katika ushindi wa 2-1 wa Mali dhidi ya Burkina Faso katika mchuano wa Kombe la Mataifa ya Afrika, ‘AFCON 2023’ kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora, Lassine Sinayoko amesema bado kuna kazi nyingi ya kufanya, licha ya kufurahishwa na matokeo hayo.

Mshambuliaji huyo anayecheza soka lake nchini Ufaransa alipongeza uimara wa timu yake dhidi ya majirani zao, lakini akaonya kwamba bado kuna kazi kubwa ya kufanywa kwani mechi zinazofuata zitakuwa ngumu zaidi.

“ilikuwa mechi ngumu sana dhidi ya timu nzuri. llitubidi kufanya kazi kwa bidii zaidi, lakini ninafurahi hatimaye tulipata matokeo.

“Bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili tusherehekee ushindi huu, lakini bado tukumbuke kuwa kuna kazi kubwa mbeleni,” amesema Sinayoko.

Mali watamenyana na wenyeji, Ivory Coast katika mchezo wa Robo Fainali mjini Bouake keshokutwa Jumamosi (Februari 03).

Mawaziri wanaojiuzuru watakiwa kuwa wakweli
Chujio la Maji Kabanga lakamilika, Kasulu kuneemeka