Rais wa Namibia, Hage Geingob (82), amefariki Dunia wakati alipikuwa akiendelea kupatiwa matibabu ya Saratani katika Hospitali iliyopo Mji Mkuu wa Nchi hiyo, Windhoek.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Makamu wa Rais wa Taifa hilo, Nangolo Mbumba imeeleza kuwa Kiongozi huyo alifariki usiku wa kuamkia hii leo Februari 4, 2024.
Hata hivyo, kabla ya kifo chake Hayati Geingob Januari 2024 alikuwa tayari ameshaweka wazi mbele ya hadhara kuhusu kusumbuliwa na maradhi ya saratani.
Hage Geingob aliapishwa kuwa rais wa Namibia mwaka 2015 na mpaka anafariki alikuwa anatumikia awamu yake ya pili na ya mwisho uongozini.
2023 alifanyiwa upasuaji wa moyo na mwaka huu 2014 aliweka wazi kuwa alipona saratani ya tezi dume.
Hata hivyo, Namibia inatarajiwa kuandaa uchaguzi wake mkuu mwezi Novemba 2024 ambapo Chama tawala cha SWAPO kilicho madarakani tangu mwaka 1990, kimemteua Bi Nandi-Ndaitwah kama mgombea wa urais.