Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi –  CCM, Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amesema maridhiano sio ya vyama vyama vya siasa pekee, bali ni ya jamii kwa ujumla katika kujenga umoja na mshikamano wa Taifa.

Kinana ameyasema hayo katika Mkutano wa Wanachama na Viongozi wa Mkoa wa Dar Es Salaam, uliofanyika hii leo Februari 4, 2024 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Amesema, “chimbuko la maridhiano lilianza Aprili 24, 2021. Maridhiano yana pacha wake, pacha wake ni ustahimilivu. Hakuna maridhiano bila ustahimilivu.”

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi –  CCM, Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana.

“Katika vikao vyote; (Baraza la Vyama, Kituo cha Demokrasia) ndugu zetu CHADEMA hawakushiriki, hawakutaka kwenda. Kikaundwa kikosi kazi hawakwenda, wengine wote walienda lakini wao hawakwenda.” aliongeza Kinana.

Aidha, ameongeza kuwa, “hoja zote tulizozijadili kwa mwaka mzima katika vikao, 11 ni hoja zilizotokana na CHADEMA hakuna hoja hata moja ya CCM. Ni uungwana gani unaotaka zaidi ya hapo?.”

Ujenzi Nyumba za waathiriwa Hanang' kuzingatia ubora, viwango
Rais wa Namibia Hage Geingob afariki Dunia