Afarah Suleiman, Hanang Manyara.

Jamii Wilayani Hanang Mkoani Manyara, imetakiwa kuutunza Mlima Hanang kwa kupanda miti pamoja na kutofanya shughuli za kiuchumi pembezoni mwa mlima huo, ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kutokea kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mwakilishi wa Shirika la ActionAid, Elias Mtinda ameyasema hayo wakati wa semina maalum iliyowakutanisha wadau wa misitu wakiwemo viongozi wa vijiji, wawakikishi wa watoto, Watendaji wa Kata pamoja na wilaya, iliyolenga kuwapa elimu namna ya kuutunza mlima Hanang, iliyofanyika Wilayani humo.

Mgeni Rasmi katika semina hiyo,  Diwani wa Kata ya Katesh na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’, William Manase amesema sababu zinazopelekea kuwepo kwa athari katika milima ni pamoja na uharibifu wa mazingira na mapitio ya maji, na kuwataka Wananchi kuutunza mlima huo.

Naye Mhifadhi Msaidizi wa Mlima Hanang’, John Masatu kutoka TFS amesema kumekuwa na changamoto zinazoukabili mlima kutokana na baadhi ya Wananchi kukata miti hovyo, kujenga na kulima kwenye hifadhi ya mlima na kuchoma misitu, hali inayopelekea mlima huo kuleta athari Kwa binadamu.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamewashukuru waandaaji na wawasilishaji wa Semina hiyo ya utunzaji wa mlima Hanang, kwani imewasaidia na wao watakwenda kuwa mabalozi wazuri kwa jamii inayouzunguka mlima huko ili kuwaelimisha.

 

CCM yahimiza umoja, mshikamano Pwani
Wapeni fomu vikao vitawajadili - Karamagi