Johansen Buberwa – Kagera.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Kagera, Nazir Karamagi amewataka makatibu wa chama hicho na watendaji wote ndani ya Mkoa kutojihusisha na vitendo vyovyote vya kuchelewesha wagombea kupatiwa fomu la sivyo watasimamishwa kazi.

Akizungumza na Wanachama, Viongozi mbalimbali wa Serikali na wananchi katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 47 ya CCM Mkoa Kagera yaliyofanyika Wilaya Muleba Mkoani humo, Karamagi amesema kwasasa wananchi wana imani na CCM, hivyo hawakotayari kuona anajitokeza Kiongozi yoyote anaye enenda kinyume na utaratibu wa chama.

“Hakuna kumwangalia mtoto wa mjomba wala mtoto wa shangazi tamko langu kwa watendaji wenzangu mwananchama yoyote atakaya kuja kuchukua fomu ya kugombea nafasi yoyote wewe kazi yako ni kumpatia fomu ajaze watakao mjadili ni vikao sio wewe,” alisema Karamagi.

Wahimizwa kutunza hifadhi Mlima Hanang'
Serikali yateta na Wawekezaji Indaba