Klabu ya Manchester United imeripotiwa imeanza kuwasiliana na makocha Antonio Conte na Julen Lopetegui kwa miezi ya hivi karibuni kwa ajili ya kuwapa kazi huko Old Trafford.

Kocha Erik ten Hag aliipa timu hiyo ya Man Unitd ubingwa wa Kombe la Ligi kwenye msimu wake wa kwanza, lakini sasa mambo yamekuwa magumu na kujiweka kwenye presha kubwa.

Kutupwa nje mapema kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kumemweka kwenye wakati mgumu zaidi kocha huyo, huku timu ikishindwa kuwamo kwenye Top Four katika Ligi Kuu ya England.

Man United kwa sasa ipo nyuma kwa pointi sita kuifikia Top Four inayotoa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya sasa kupata ushindi kwenye mechi mbili mfululizo dhidi ya Wolves na West Ham.

Kocha huyo Mdachi, kwa sasa ana mtihani mzito wa kumshawishi tajiri mpya, Sir Jim Ratcliffe ili asifikirie mpango wa kuleta kocha mpya.

Kinachoelezwa, Man United inafikiria kuleta kocha mpya kutokana na mwenendo wa Ten Hag.

Kwenye orodha ya makocha wanaotajwa ni Conte na Lopetegui na kuona kama watakuwa tayari kwenda kupiga kazi The Theatre of Dreams.

Kinachoelezwa kama kutakuwa na mabadiliko yoyote basi itakuwa mwishoni mwa msimu huu.

Conte aliongoza Tottenham kwenye mechi 77, akishinda 41, lakini amekutana na vipigo 24 vilivyomfanya afunguliwe mlango wa kutokea huko kwa wababe hao wa London.

Kocha Lopetegui aliachana na Wolves, Agosti mwaka jana baada ya timu hiyo kushindwa kusajili wachezaji aliowataka kufuatia kubanwa na sheria ya FFP.

Pombe haramu yauwa sita, watano wapoteza uoni
Saido, Onana wapewa salamu Simba SC