Takribani Watu sita wamefariki dunia, huku wengine watano wakidaiwa kupoteza uoni kwa muda, baada ya kudauwa kunywa pombe haramu Katika baa ya California iliyopo Mtaa wa Mwea Magharibi, Kaunti ya Kirinyaga Nchini Kenya.

Mtendaji wa kaunti ya Kirinyaga, George Karoki amesema huenda waathiriwa hao walichanganya dawa ya Ethanol na pombe hiyo kali, ambayo iliyosababisha uoni hafifu na ugonjwa wa ini.

Amesema, mara baada ya tukio hilo, watu hao waliopoteza uoni, walikimbizwa katika Zahanati iliyokuwa karibu ambapo walitibiwa na kuruhusiwa.

Inadaiwa kuwa watu hao waliofariki walifikishwa katika Zahanati, lakini hawakuweza kupata huduma hivyo kukimbizwa katika Hospitali Kuu ya Kerugoya ambapo walifariki baadaye.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 7, 2024
Ten Hag yupo kikaangoni Man Utd