Mkuu wa Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani Nchini, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Michael Deceli amewataka madereva wa vyombo vya moto kuzingatia alama za barabarani, ili kupunguza ajali kwa watumiaji wengine wa barabara.

Akizungumza baada ya kuhitimisha utoaji wa elimu ya uvukaji wa barabara kwenye vivuko vya waenda kwa miguu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Misugusugu Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani, Deceli amesema kumekuwepo na baadhi ya madereva wa vyombo vya moto wakiwemo madereva wa Serikali kutokusimama kwenye vivuko vya waenda kwa miguu na kupelekea ajali katika baadhi ya maeneo.

Amesema, “suala la kuheshimu alama za barabarani ni la kila dereva anayeendesha chombo cha moto, Sheria haijabagua madereva wa kuziheshimu alama hizo na wengine kutokuheshimu.”

Deceli pia amewataka madereva walioweka magari yao ving’ora pasipo kuwa na kibali cha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kuondoa mara moja na wale watakao kamatwa wakiwa hawana vibali hivyo, watachukuliwa hatua za kisheria.

Mo Dewji kusimamia usajili Simba SC
MALIMWENGU: Ukiruka kichurachura mara 20 unasafiri bure