Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda amekemea tabia ya baadhi ya Viongozi walioaminiwa na kupewa Wizara kutofanya kazi ya kumsadia Rais na badala yake hutengeneza makundi ya watu kuwasifia na kusababisha uzembe kwa watendaji wa ngazi ya chini, hali inayopelekea Wananchi kutohudumiwa na kutopata maendeleo kwa wakati.
Makonda ameyasema hayo wakati akisalimiana na kuzungumza na Wananchi wa Mji mdogo wa Laela akiwa njian kuelekea Mkoani Songwe katika muendelezo wa ziara yake ya Mikoa 20ya kusikiliza kukagua na kutatua changamoto mbalimbali za Wananchi.
Amesema, “mimi wala sihitaji Viongozi wa Serikali wasiofanya kazi wanipende kwa madudu yao, ziara hizi tunazofanya CCM titaeeka bayana kila sekta ili kuona kazi inafanyika au laa wapo baadhi ya Viongozi wengine wameaminiwa na kupewa Wizara badala ya kufanya kazi walizopewa wao wanahangaika kutnegeneza watu wa kuwasifia badala ya kuwasimamia watendaji wao huku chini maana mambo hayaendi vema sehemu nyingi.”
“Uzuri ni kwamba mimi siogopo kuchukiwa wala kusemwa na bahati mbaya mimi sio muoga yani siogopi chocjote na nimeapa sitamdanganya Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan , lazima nimwambie ukweli sehemu yoyote nikikuta madudu yoyote,” alisema Makonda.
Aidha ameongeza kuwa, “Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia ametoa fedha nyingi za miradi mbalimbali ya maendeleo nchi nzima katika kila Wizara kila Sekta lakini baadhi ya Viongozi hawasimamii kwa kufuatilia na matokeo yake wanampelekea taarifa Mhe. Rais kwamba mambo yapo sawa kumne chini huku Wananchi wanateseka , hilo kwangu kupitia ziara hizi sitalifumbia macho.”