Watu wawili wamefariki na wengine wanne kujeruhiwa, akiwemo Dereva wa Gari la Wagonjwa pamoja na mgonjwa aliekuwa akisafirishwa kutoka Hospitali ya Korogwe kuelekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo, kwa ajili ya matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo chake ni uzembe wa Dereva wa Lori aliyekuwa akijaribu kuyapita magari mengine katika eneo lisiloruhusiwa.

Amesema, ajali ilihusisha Gari hilo la Wagonjwa lenye namba za usajili SM 9046 liligongana uso kwa uso na Roli la mizigo aina ya Scania lenye namba usajili T262 ALT eneo la Chang’ombe lililopo Wilayani Handeni, Mkoani Tanga.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mji wa Korogwe, Dkt. Heri Kilwale amekiri kupokea miili miwili ya marehemu ambayo imehifadhiwa hospitalini hapo pamoja na majeruhi wanne ambao wamepelekwa Hospitali ya Mkoa kwa matibabu zaidi.

Serikali kuwekeza nguvu Teknolojia mbadala ujenzi Barabara za Wilaya
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 9, 2024