Lydia Mollel – Morogoro.

Wanawake waliopo kwenye ndoa wametakiwa kuacha kutunza siri ya kile wanachokipitia ili kulinda heshima ya familia zao kwa dhamira ya kufia ndoa badala yake watoe taarifa endapo vitendo vya Unyanyasaji na Ukatili vitakithiri ili hatua stahiki zichukuliwe.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Malinyi, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Michael Rasha alipotembelea wodi ya wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Malinyi kwa ajili ya kutoa msaada na kuwapa elimu.

Amesema, ni muhimu kuvumilia madhira yaliyopo kwenye ndoa ili kulinda lakini ikifikia wakati unafanyiwa Ukatili usisite kutoa taarifa, kwa kufanya hivyo itakusaidia kuwa salama na kuimarisha ndoa yako.

Aidha, Mkaguzi huyo amesisitiza juu ya malezi bora kwa watoto ili kuwa na kizazi chema ambacho kitauchukia uhalifu na kufanya yale ambayo Sheria na taratibu za nchi zimeelekeza.

Kwa upande wake Sajenti wa Polisi Mwanaisha ambaye aliambatana na Mkaguzi huyo ametoa elimu juu ya madhara ya mimba za utotoni, lishe bora kwa mtoto na mama aliyetoka kujifungua, madhara ya ukatili kwa watoto pamoja na kutojichukulia sheria mkononi.

Ondokeni mabondeni kupunguza maafa - Majaliwa
Serikali kuwekeza nguvu Teknolojia mbadala ujenzi Barabara za Wilaya