Ikiwa imefika Miezi miwili tangu Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kuanza masomo yao, hali imekuwa tofauti kwa Mtoto Japhary Kasimba (7), ambaye amefikia umri wa kwenda shule kutokana na kuto kuandikishwa na wazazi wake kwa kisingizio cha hali duni ya maisha.

Hali hiyo imemshangaza Mkuu wa Dawati la Jinsia Wilaya ya Malinyi, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Michael Rasha alipomkuta Mtoto huyo machungani na baba yake na kupelekea kuchukua hatua ya kuzungumza na mzazi huyo juu ya umuhimu wa shule na kumpa maagizo ya kumuandikisha shule haraka.

Samweli Kasimba ambaye ni baba mzazi wa Japhary alipoulizwa kwanini hakumpeleka mtoto shuleni, alijibu kuwa sababu ni kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za shule ambazo ni sare pamoja na madaftari, ambapo Mkaguzi Rasha akamshauri mzazi huyo kutafuta pesa, ili amnunulie mahitaji ya shule mtoto huyo kwani anayo ajira inayomuingizia kipato.

Amesema ni lazima mtoto huyo apewe haki yake muhimu ya elimu hivyo ataendelea kumfuatilia na kumuhimiza mzazi huyo achukue hatua za haraka kwani kitendo cha kuwafanyisha watoto kazi bila kukumbuka kuwapa elimu ya msingi ni kuharibu Taifa la kesho ambayo itasaidia kuwajengea uwezo wa kujielewa na kujitambua.

“Ni jambo la kushangaza mpaka leo kuona bado kuna wazazi/walezi hawajui umuhimu wa elimu na kuwafanyisha shughuli mbalimbali watoto wao ambao wanapaswa kuwa shuleni kwa wakati huo, Sisi kama Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Malinyi tutahakikisha tunawafikia watoto wote wenye changamoto hii na kuongea na wazazi wao ili kupata kizazi cha baadae kilichoelimika” alisisitiza Rasha.

Haaland: Man City haitaweza tena
Uhaini: Serikali kuwarejeshea adhabu ya kifo waasi