Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameamuru Wanajeshi wake 2,900 kupelekwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo – DRC, ili wakasaidie kupambana na waasi.

Wanajeshi hao, wataelekea DRC wakiwa ni sehemu ya Majeshi ya Kusini mwa Afrika kwa Kongo (SAMIDRC), walioidhinishwa Mei 2023, wakichukua nafasi ya mejeshi ya Afrika Mashariki ambayo yaliondoka DRC Desemba 2023, baada ya kudaiwa kukosa ufanisi.

Hatua hiyo, inakuwa wakati ambapo mapigano yakiendelea Mashariki mwa Kongo na kusababisha maelfu ya watu kuongeza idadi hadi kufikia milioni saba ya waliolazimika kuondoka katika makazi yao kutokana na mizozo.

Msiba huu si wa familia yetu pekee - Fred Lowassa
Picha: Matukio mbalimbali katika zoezi la kuaga mwili wa Lowassa