Fred Lowassa, ambaye ni Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa bega kwa bega na familia kipindi ambacho walikuwa wakimuuguza baba yao.

Fred ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, amesema Rais Samia alikuwa akiulizia hali ya Baba yao kila baada ya nusu saa hadi mauti yalipomkuta, huku akisema msiba huo si wa familia yao pekee bali ni wa Watanzania wote kutokana na uhalisia wa watu wengi kuguswa na kifo cha Kiongozi huyo.

Amesema, “tumesikia maneno mengi ya upendo na historia kutoka kwa viongozi wetu na yametufariji sana, baba alipata mauti siku ya jumamosi, kwakweli tunalipokea hili kwa amani. Lakini katika vita yake hii ya kupigania uhai kwa kipekee wacha nitoe shukrani zetu kwa Mama Samia tunamshukuru sana kutoka moyoni.”

Aidha, Fred ameongeza kuwa, “Siku Rais anasafiri kuelekea Italy, alimtuma Mkuu wa Majeshi na alikuwa akiulizia hali yake kila baada ya nusu saa, kiukweli nasema asante sana tena sana nawashukuruni nyote.

MAKALA: Wanyama 10 wenye akili zaidi Duniani
Ramaphosa apeleka kikosi kazi kuwakabili M23