Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameungana na ndugu, jamaa na marafiki kwenye mazishi ya aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Ibrahim Msabaha (72) aliyefariki dunia Jumanne, Februari 13, 2024.
Kikwete alihudhuria mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu Kibaha, Mkoani Pwani, akiambatana na nugu, jamaa na marafiki wa familia ya Dkt. Msabaha katika kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele.
Hayati Dkt. Msabaha alifariki dunia akiwa njiani akipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, baada ya hali yake kubadilika ghafla ikiwa ni siku chache tangu atoke Hospitali hapo alikokuwa amelazwa.
Dkt. Msabaha amewahi kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Kibaha, Mkoani Pwani kupitia Chama cha Mapinduzi – CCM.

Mgao wa umeme kumalizika Machi, majaribio yakamilika
Watatu wasimamishwa kazi kwa utoro, wawili kikaangoni