Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza malezi bora katika jamii ili kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya, wizi, ubadhirifu wa mali za umma, udhalilishaji na ulevi.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa Msikiti wa Makuti Kisiwandui Mkoa wa Mjini Magharibi  hii leo Februari16, 2024.

Amesema, malezi bora yanaanzia ngazi ya familia, pia amewataka wazazi na walezi Kuwalea vijana katika malezi mema yenye maadili.

Rais Dk.Mwinyi ameshiriki katika ibada ya sala ya Ijumaa Misikiti mbalimbali Unguja na Pemba mpaka sasa idadi yake ni 133 pia amefungua Misikiti mipya 28 Unguja na Pemba.

Vijana waaswa kutowakaribisha Watoto vijiweni
Mgao wa umeme kumalizika Machi, majaribio yakamilika