Vijana wanaoshinda vijiweni wakipiga soga na kubadilishana mawazo juu ya mipango na muelekeo wa maisha yao, wametakiwa kuto wakaribisha Wanafunzi na Watoto chini ya miaka 18, ili kuwaepusha na matendo mabaya yanayofanywa na baadhi yao.

Hayo yamebainishwa na Polisi Kata wa Kata ya Lipangalala, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Ibrahim Hassan wakati akizungumza na Vijana hao wa kijiwe cha Mkuya kilichopo Kata ya Lipangalala Wilaya Kilombero.

Amesema, “ni jambo baya na la hatari vijana wa vijiweni kukusanyika na watoto kwa sababu watoto hawa hawana chujio la kipi wajifunze kipi kibaya wakiache, wataondoka hapa na matusi, tabia za uvutaji na wizi jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao ya baadae.”

Aidha, amewataka pia kupinga ukatili wa Kijinsia na watoto, kuepuka matumizi ya dawa za kulevya, kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu pamoja na kuwapa elimu za mada mbalimbali za usalama wa raia.

Sudi Jumanne Mkazi wa mtaa huo, amesema, kama muwakilishi wa vijana wanaokaa katika kijiwe hicho wataanza kuwafukuza watoto wanaokaa hapo na kuwahimiza kukaa nyumbani na wazazi wao pindi wanaporudi shuleni.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 17, 2024
Rais Dkt. Mwinyi ahimiza malezi bora katika jamii