Maafisa Elimu Kata, Waalimu wa shule za Awali, Msingi na Wakuu wa Shule za Sekondari Wametakiwa kutumia Elimu ya TEHAMA ili kuleta tija katika kipindi hiki Cha Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Rai hiyo, imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya awali na msingi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwalimu Suzan Nussu wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa watumishi wa Kanda ya Ziwa yaliyofanyika jijini Mwanza.
Amesema, Watumishi hao wanatakiwa kuhakikisha vifaa vya TEHAMA vinatunzwa ipasavyo na vinatumiwa kwa malengo yaliyo kusudiwa kwani lengo kuu ni kuongeza ubunifu kwa wanafunzi na waalimu ili kuendana na Kasi ya Dunia ya Sasa.
Nussu ameongeza kuwa, kupitia Miradi Miwili inayofadhiliwa na mkopo wa Benki ya Dunia yaani Sequip kwa Shule za Sekondari na BOOST Shule za Msingi imesaidia kuongeza Miuondombinu ya shule ikiwemo Madarasa na Matundu ya Vyoo.
Aidha, amebainisha kuwa kwa mwaka wa fedha unaoendelea Serikali inajenga shule 212 za Sekondari na Shule 6 za Kitaifa za Wasichana mpya kabisa na kupitia BOOST wamejemga shule 320 ili kupunguza msongamano wa Wanafunzi na kutembea umbali mrefu kufika shuleni.
Kwa uoande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Mwalimu Esther Simba ambaye ni Afisa elimu kata ya Sola, amesema kupitia elimu waliyoipata wanakwenda kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi na ufanisi makazini kwa kuwajengea uwezo waalimu wengine.