Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amekutana na kuzungumza na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Udhibiti wa huduma za Nishati kwa nchi za Afrika Mashariki – EREA, Dkt. Geoffrey Mabea.

Kikao hicho kilichofanyika hii leo Februari 26, 2024 jijini Dar es Salaam, kimejadili masuala mbalimbali ya nishati kwa nchi wanachama na umuhimu wa kujenga uwezo wa Wataalam katika Sekta ya Nishati, ili kuongeza tija na huduma bora kwa wananchi.

Aidha, kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Zanzibar, Shaib Kaduara na Wataalam kutoka EREA.

Gamondi- Haikuwa rahisi kihivyo
Tehama itumike kuleta tija Kiteknolojia - Mwl. Nussu