Jumla ya kilometa 250 za Barabara zinatarajiwa kujengwa Mkoani Dar es Salaam kwa kiwango cha lami, kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Jiji – DMDP, awamu ya pili.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila wakati wa ziara yake Wilayani Ubungo ya kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.

Amesema Serikali tayari imesaini shilingi 988 Bilioni, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo na kwamba Ubungo ni miongoni mwa maeneo yatakayonufaika na mabilioni hayo huku akiwataka wananchi kuunga mkono jitihada hizo.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba alisema Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo pia  imetenga kiasi cha shilingi 1.8 Bilioni zitazotolewa kukarabari barabara ambazo haziko katika utaratibu wa TANROAD na TARURA.

Tehama itumike kuleta tija Kiteknolojia - Mwl. Nussu
Mpambanaji ametangulia: Pumzika Hage