Diwani kata ya Bahi Mkoani Dodoma, Augustin Ndonu amekemea vikali tabia ya baadhi ya Wananchi wa kata hiyo kutaka kufanya maandamano ya siri wakilalamikia kukatika kwa moja ya barabara inayounganisha Kata hiyo.
Akizungumza na Dar24 Media hii leo Jijini Dodoma, Ndonu amesema tabia ya kutaka kuleta mtafaruku kwa watu sio nzuri na yeyote anayetaka kufanya hivyo atapata taarifa na hivyo atachukua hatua za kisheria dhidi yake.
Amesema, “Kiongozi wenu najitambua na Wiki iliyopita nilikuja na watu wa Tarura kwaajili ya kupima na kuweka pesa ili ujenzi wa kurekebisha barabara hiyo hianze mapema sana, kwaio niwaondoe tu wasa wasi kuwa urekebishaji wa barabara utaanza hivi karibuni”. Amesema Ndonu
Katika hatua nyingine, Diwani Ndonu amesema kupitia Idara ya Kilimo na Uvuvi ya Halmashauri hiyo ya Bahi, wamelifungia Bwawa la Samaki kwa muda wa miezi mitatu ili waweze kuzaliana na kukua.
Amesema, “tulikaa na kushauriana na mtaalamu alileta wazo hili la kulifunga Bwawa kwa muda wa miezi mitatu na mimi kama Diwani nikaunga mkono kutokana na kuwapa nafasi Samaki wanao patikana hapo kukuwa vizuri, ili tunapokuja kufanya biashara basi kila mmoja ananufaika vizuri.”
“Lakini pia tunataka kuepusha uvuvi haramu ambao ulikuwa unaendelea hivi karibuni, tunajua Wananchi ndio wanufaikaji wa bwawa hili hivyo tuwape nafasi mifugo yetu ikue vizuri ili tunapokuja kuvua na kuwauza basi faida iwe kwa kila upande,” amesema Diwani Ndonu.