Mfugaji mmoja Jamii ya Kimasai, Kombeti Kalaita anadaiwa kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na Mlinzi wa SUMA JKT, baada ya kuingiza mifugo katika Shamba linalolindwa na askari hao katika Kijiji cha Ilonga kilichopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.

Majeruhi huyo, amesema siku ya tukio wakiwa wanachunga mifugo walipofika katika mto ulio karibu na shamba hilo, Askari hao wakachukua mifugo hiyo na kuiepeleka eneo jingine na kuwajeruhi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema tayari mlinzi mmoja anashikiliwa kwa ajili ya mahojiano.

Amesema chanzo cha tukio hilo ni Wafugaji hao kutaka kuwashambuliwa Walinzi kwa silaha za jadi wakitaka kuchukua mifugo iliyokamatwa kinguvu ndipo askari huyo akajihami.

Dkt. Mpango: Chukueni maoni ya Wafanyabiashara
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 28, 2024