Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Shule ya uongozi ya Mwalimu Julias Kambarage Nyerere ya Kibaha Mkoani Pwani, imewakutanisha wawakilishi wa Chama cha Kikomunisty cha China – CPC, na Wataalamu wabobezi toka vyuo vikuu kadhaa nchini, kujadili maboresho ya mahusiano ya kimaendeleo ili kunufaika kiuchumi kupiga hatua za Maendeleo.

Semina hiyo ya siku moja imefanyika Shuleni hapo ambapo Wataalamu hao walijadili namna ya kufanya maboresho katika sekta ya kilimo, uvuvi, utalii na ujenzi ili Tanzania na Afrika kwa ujumla tuendelee kunufaika na uhusiano wa nchi ya China na Chama Cha CPC.

Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julias Kambarage Nyerere Prof. Macelina Chijoriga amesema yapo mambo kadhaa mazuri ya kujifunza sisi taifa la Tanzania yakiwemo masuala ya ya uchumi na ya kijamii toka nchini China ilikujua namna China walivyofanikiwa tangu walipotokea kimaendeleo kuanzia miaka ya sitini hadi kufikia hatua iliyopo hivi sasa ambapo tulifanana kiuchumi.

Naye Mwakilishi wa Chama cha kikomunisty cha nchini China CPC, Jin Xin amesema China wamekuwa na ushirikiano na nchi za Africa kwa kuimarisha mawasiliano na mahusiano na kwamba wanamengi ya kushirikiana na Tanzania na Bara Zima la Afrika katika sekta ya kilimo, uvuvi, utalii na miundombinu.

Amesema kujengwa kwa Shule hiyo ya uongozi ya Mwalimu Julias Kambarage Nyerere kwaajili ya Vyama sita vya harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa ni Moja ya mfano mzuri wa Tanzania na nchi ya China.

Kwa upande Kanali mstaafu George Simbakaria amesema jambo mojawapo la kujifunza ni namna walivyotengeneza vizazi vyenye uadilifu kuanzia utotoni akidai ili kutoa viongozi bora ni lazima malezi ya watoto na vijana kwakulelewa toka chini kuwa waadilifu na waaminifu kwa taifa lao na sio kuendeleza vitendo vya kutokuwa na uwaadilifu na uaminifu kwa taifa letu.

Amesema, jambo kubwa la kujifunza kwa China ni kwamba mafanikio yake hayakutokana na ukoroni kama ilivyokuwa katika mataifa mengine makubwa ambayo yaliwahi kutawala katika koloni mbalimbali barani Africa na mataifa mengine duniani.

Awali, Mkuu wa Kituo cha tafiti za uchumi na jamii nchini Dkt. Hoseana Lunogelo amesema nchi ya China shughuli zake za kimaendeleo na shughuli za chaguzi hazina kabisa tuhuma za rushwa hivyo tunaweza kujifunza kwao namna ya kuboresha na kudhibiti vitendo vya rushwa katika taifa letu na Bara Zima la Afrika.

Naye Mhadhiri toka Chuo cha Mwalimu Julias Kambarage Nyerere Nyerere Kampasi ya Zanzibar, Dkt Rose Mbwete aliongeza kuwa Watanzania wana vingi vya kujifunza kutoka taifa la China ili watanzania kufikia hatua ya maendeleo kama nchi ya China iliyo nafasi ya pili duniani ni kufanya kazi kwa bidii na kuwa na miongozo dhabiti inayodhibiti vitendo vya rushwa.

 

Dkt. Biteko: Utamaduni, utu wa Mtanzania usidhalilishwe
RC Telack: Lindi, Kilwa jiandaeni kuwapokea Watalii