Takribani Watu 44 wamefariki na wengine ambao idadi yao haijajulikana mara moja wakijeruhiwa baada ya moto kuteketeza jengo la ghorofa saba katika kitongoji kimoja cha mji mkuu wa Bangladesh.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Inspekta Mkuu wa Polisi, Bacchu Mia alisema aqali kulikuwa na vifo 33, lakini mtu mwingine alifariki akiwa Hospitali ya Polisi ya mjini Dhaka na kufanya idadi ya vifo kufikia 44.
Awali, Waziri wa Afya wa Bangladesh, Samanta Lal Sen baada ya kuitembelea Hospitali ya mjini Dhaka ya Medical College Hospital, alisema watu 43 ndiyo waliofariki kutokana na Moto huo.
Kwa upande wake Afisa wa Idara ya Zimamoto, Mohammad Shihab alisema moto huo ulianzia katika mgahawa maarufu wa biriyani kwenye barabara ya Bailey mjini Dhaka Februari 29, 2024 na kusambaa haraka hadi kwenye ghorofa za juu.