Sina shaka utakuwa umeshawahi kulisikia jina la Pomboo, huyu ni Mnyama ambaye ana sifa za kustaajabisha na wengi wenu mnamfahamu kwa jina la lugha ya kigeni yaani Dolphin.

Pomboo ni jamii ya Samaki lakini anazaa na kunyonyesha, lakini anapozaa huanza kumtoa mtoto mkia na si kichwa. Sifa yake kubwa ni kuwa na kasi kubwa sana majini na hupendelea kucheza muda mwingi na mdomoni ana meno yapatayo 100 wakiwa na namna yao ya kuwasiliana kwa lugha tena kwa sauti, pia ni kiumbe mpole na mwenye akili myingi.

Urafiki na Binadamu.

Ni ngumu sana kwa viumbe hawa kuwa na urafiki baina yao wanyama ya makundi tofauti, walioliweza hili ni mamba na kiboko tuu, lakini hapa anajitokeza  Pomboo, kiukweli huwezi kufa maji kama Samaki huyu anakuona unatapatapa ni muokoaji kabisa, lakini pia huwezi kupata madhara ya kushambuliwa na Samaki wakali kama papa, halafu Pomboo akakuacha kwani atakulinda kwa hali na mali.

 

Inapotokea umedumbukia majini na akakuona haraka sana hukufikia, kisha atakukumbatia na kwa spidi kubwa atakuwa anakupeleka nchi kavu, atakapofika jirani atakachokifanya ni kukurusha nchi kavu na msaada wake unakuwa unaishia hapo, ukitua kwenye jiwe, mwamba, michongoma, mtini shauri yako yeye kazi yake ashamaliza, pole utapewaga na wasamaria.

Upo ushahidi pia kuonesha ya kwamba Pomboo kuwahi kuwasaidia watu katika mazira mbambali kama hayo, kuna hadithi kuwa siku moja kuna Meli ilipita ukanda wa Samaki hao, kisha wakaanza kuifuata, nahodha mmoja alipotambua Pomboo wanafuatilia chombo chake alimua kusimama, ili aweze kuwatizama vyema.

Michezo.

Michezo waliyofanya Pomboo wale ilimhamasisha Nahodha kuingia majini ili aoge nao, unajua wezentu wazungu tena alimuona Pomboo anarudi kinyumenyume, akajumuika nao majini, pasina ya kujua eneo hilo lilikuwa samaki mkorofi papa, hata hivyo pamoja na kujeruhiwa Pomboo walihakikisha wanamlinda Nahondha huyo kwa kumzingira.

 

Kisha wakawa wanatoa sauti za kumkaripia Papa, mpaka papa huyo alipoondoka kwa hasira, Pomboo wakamaliza kazi kwa kumrudisha nahodha huyo katika chombo chake kisha wao wakaendelea na mambo yao.

Hata hivyo, inaarifiwa kuwa Pomboo ndiye mnyama mwenye akili kuliko wote baada ya binadamu, Wanasayansi walibaini ya kwamba Pomboo wanatambua ala za mziki na wakiusikia wanaweza kabisa kuucheza na kuna kipindi kuna mipango ilianza kuratibiwa ili kuwafungia spika za mziki wa blues ili waweze kuzaliana zaidi.

Wanalindwa.

Ni Samaki anayelindwa na Umoja wa Mataifa, lakini pamoja na wema wote huu wa Pomboo bado Binadamu wasio wema kwake humuwinda na kumuua.

Pomboo pia huwasaidia Wavuvi katika harakati zao zao za uvuaji wa Samaki, kwa kutumia mkia wake ambapo huwapiga Samaki wakubwa na hapo wavuvi hufanikisha upataji wa Vitoweo vya kutosha na huwa Pomboo wanafanya hivyo kwa mapenzi aliyonayo kwa Wanadamu.

Anthony Joshua atamba kumchakaza Ngannou
Neymar atamani kucheza Marekani