Muziki ni aina ya sanaa inayotumia sauti mbalimbali za kibinadamu na zile za ala, ambapo inaweza kuwa kwa pamoja au kila moja pekee. Asili ya neno Muziki ipo katika lugha ya Kigiriki na kipindi hiki uliitwa Mousikee.

Baadhi ya sifa za muziki ni uzito wa sauti na uzani au mahadhi ambapo aina ya Muziki inayopatikana kote duniani ni nyimbo ambazo ni maneno yanayotolewa kwa sauti na mahadhi ya aina tofauti vikiwa na ala.

Kwa wale wanaorekodi sauti, wao huenda studio kurekodi na huchukuliwa kwa kinasa sauti kilichoambatanishwa na tarakilishi na kudhibitiwa na kompresa kisha tunapata ladha yenye mchanganyo halisi tukiuita MUZIKI.

Unapendwa sana na Walimwengu karibia wote lakini kama ujuavyo, kwenye maharage arobaini hukosi harage moja bovu kwani wasioupenda pia wapo, najua hili linaweza kukushangaza.

Hussein Bangege ni kijana kutoka Kigoma, aliupenda sana Muziki kukiko chakula japo asingekua najua unaelewa nini kingetokea na labda angekuwa amefutika Duniani, ambaye aliuishi Muziki kwa takribani miaka 20 bila dalili ya kufanikiwa japo yeye aliamini angeweza kuja kuwa mtu maarufu nchini kama si Duniani lakini haikuwezekana.

Aliishi na Bibi yake baada ya kupoteza wazazi wake akiwa na umri mdogo, hata kipaji cha huo Muziki alikirithi kwa Baba yake ambaye alikuwa ni mwimbaji na mpiga Gitaa maarufu huko Kasulu, na wakati akitafakari nini afanye ili aweze kutimiza ndoto yake, kila kukicha viliibuka vipaji vipya na akikumbuka na miaka 13 hajakanyaga kwa bibi yake akidai anajitafuta hivyo simu ilihusika sana kimawasiliano.

Desemba 2023 akaona huenda alipoteza bahati na baraka kutoka kwa Bibi yake kwa kutokuonana naye akikimbiza miongo miwili, hivyo akaona bora aende kutubu, kufika alikutana na mlezi wake huyo Bibi Mafuru, anadai kwanza bibi alimpiga bonge la kofi akimtuhumu kukaa nje ya nyumbani kwa muda mrefu.

Hussein ambaye kwa huku Dar es Salaam alifahamika kama Chuse Boy anadai kwamba kilichofuata Bibi hakurudi kwani alilala msibani hivyo mchana wa kesho yake aliporudi walisalimiana na kupeana habari nyingi sana za furaha na huzuni, punde Bibi alimtaarifu kuwa anaenda kumuandalia chakula na akimuahidi awe na subira ili wapeane habari nyingi zaidi na kuweka mikakati mipya.

Wakati huu Hussein alikuwa amekaa chini ya Mwembe akitafakari namna ambavyo alipumzika hapo kipindi ametoka jandoni akiwa na rafiki zake, hisia zikamuijia kwamba achukue Gitaa lake alilotoka nalo mjini ili aweze kutengeneza mashairi mapya maana akili yake ili kuwa imepata kupumua.

Anasema, “nikaingia chumbani kwangu Gitaa halipo, nikadhani labda nililiacha sebuleni pia sikulikuta basi nikaona nimuulize Bibi huenda labda alilihamisha, ile kufika jikoni anapopika nakuta kalivunja amelichocheka katika moto anaimba nyimbo za kiha huku akitabasamu.”

“Nilipiga yowe kushangaa jembe langu leo linaivisha ugali, lakini Bibi akaniambia eti kwa kizungu tena kwa mbwembwe I HATE MUSIC, halafu akasema hata baba yako alipotea kwa ujinga kama huu, kitoto kidogo miaka 13 ndio unaduri nyumbani tena huna hata hela, halafu akanitukana.”

Anasema, badala ya kulia alianza kucheka huku Bibi naye akamsaidia na kumuambia kwamba kesho yake waende akamuoneshe shamba huo ndio utakuwa Muziki wake mpya ndipo akakumbuka wakati anaondoka Bibi yake alimuambia “Hussein mjukuu wangu unaupenda Muziki ila wenyewe haukupendi.”

Msiwafunge Biashara, wapeni elimu ya kodi - Meya Kagera
Hugo Broos: Tulistahili kucheza fainali