Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Katika kuelekea siku ya Wanawake Dunia Machi 8, Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa Manyara wamesherehekea siku hiyo na Wanawake wa kata ya kaiti Kijiji Cha Minjingu Wilaya Babati Mkoani humo, ikiwa ni pamoja na kuwapatia zawadi ya vyakula.

Akizungumza katika sherehe hizo Mgeni Rasmi ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa Manyara, SACP, Geogre Katabazi amewapongeza Wanawake kwa siku yao hiyo muhimu.

Naye Mwenyekiti wa Mtandao huo Mratibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi ambaye pia ni OCD wa Wilaya Hanang, Amina Kahando amesema katika kilele cha siku hiyo, wamewashika mkono na kula nao pamoja na Wanawake hao, ili kujenga ukaribu na ushirikiano na jamii.

Kwa upande wao baadhi Wanawake wa Kijiji cha Minjingu, wamelishukuru Jeshi la Polisi kupitia mtandao huo wa Wanawake Polisi kwa kuwakumbuka kuungana nao na kuwapatia chakula kwa ajili ya familia zao.

Dkt. Mfaume: Watumishi wa Afya fanyeni kazi kwa weledi
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 7, 2024