Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta amemsifia Mlinda Lango wake, Aaron Ramsdale kwa ukomavu aliouonyesha baada ya kufanya makosa yaliyozalisha bao kwenye mchezo wao dhidi ya Brentford uliomalizika kwa washika mitutu hao kūshinda mabao 2-1.

Ramsdale ambaye amekuwa hapati nafasi ya kutosha tangu kuanza kwa msimu huu, baada ya Arteta kuonekana kumwamini zaidi David Raya, alipewa nafasi ya kuanza kwa sababu sheria za mkataba wa mkopo wa Raya hazimruhusu kucheza mechi dhidi ya Brentford ambako ndiko alikotoka kwa mkopo.

Baada ya kupewa nafasi, mambo yalionekana kuwa magumu kwa kuruhusu bao la Yoane Wissa lililokuwa ni la kusawazisha baada ya washika mitutu hao kupata bao la kwanza lililofungwa na Declan Rice.

Rasmdale aliruhusu bao hilo kwa kushindwa kuuchezea vizuri mpira aliorudishiwa na Ben White kiasi cha kumruhusu Wissa amfikie na kuupiga kwenda golini.

Hata hivyo, Arterta amesema ana furaha sana kutokana na kile ambacho kimeonyeshwa na kipa huyo ambacho yeye anakiita ni ujasiri.

“Makosa ni sehemu ya soka, kikubwa ni namna unavyofanya baada ya makosa, hususani kwa makipa ambao ndio wanacheza eneo la hatari zaidi, yeye alionyesha ukomavu sana, sijashangazwa sana kwa sababu timu nzima na uwanja mzima ulikuwa nyuma yake, alipewa heshima na tulihitaji kushinda kwa ajili yake.

Arsenal kwa sasa ipo katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England na baada ya ushindi huo imefikisha pointi 64 na kukaa kileleni, huku Liverpool na Manchester City zikitoka sare ya 1-1, katika mchezo wa jana Jumapili (Machi 10).

Pascal Wawa ageukia ukocha
Wazalendo huru wawagusa Wanawake wafungwa