Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Jukwaa la Wazalendo huru mkoa wa Pwani Waadhimisha siku ya Mwanamke duniani kwa kwenda kupeleka msaada wa mahitaji mbali mbali nuhimu katika Gereza la Wanawake la mkoa wa Lindi kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhudumia wananchi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kibaha kabla ya kuanza safari ya kwenda kupeleka msaada huo, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wazalendo Huru Tanzania, Khadija Juma amesema katika kuhakikisha uzalendo unasambaa nchini, hufanya matukio mbalimbali yatakayoonesha uzalendo katika Taifa la Tanzania.

Amesema wamekuwa wakiigusa jamii kwa namna tofauti ikiwa ni pamoja na kusaidia watoto yatima, wazee, waliopo magerezani, waathirika wa dawa za kulevya na kuhamasisha uzalendo zaidi kwa lengo la kuhakikisha watanzania wote tunakuwa wazalendo. Nakuendelea kuunga mkono serikali yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anayoyafanya ili taifa liwe salama.

“Tunahakikisha tunaigusa jamii kwa namna tofauti ili twende pamoja ili taifa letu linakuwa salama hivyo katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani tunatoa msaada wa mahitaji muhimu kwa wafungwa wakike waliopo katika gereza la mkoa wa Lindi”

Hadija alisema, “Kundi la wafungwa Wanawake ni miongoni mwa makundi yaliyosahaulika katika jamii hivyo wao waliaamua kuandaa misaada ya vitu mbalimbali ili kuwapelekea wafungwa wakike walipo katika gereza hilo ilikuonyesha upendo kwao katika siku hiyo muhimu kwa wanawake duniani.”

Aidha, ameongeza kuwa taasisi hiyo ilianzishwa kwa lengo la enzi waasisi wa taifa hili kuunga mkono kazi nzuri zinazofanywa na viongozi wa taifa letu la Tanzania katika awamu zote sita.

Amewaomba Wanawake kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia katika masuala mbalimbali anayofanya yakuendeleza taifa, huku Mwenyekiti wa jukwaa la wazalendo huru Mkoa wa Pwani, Ivan Rutatina akisema jukwaa hilo katika mwezi huu wa kuonyesha upendo kwa kudi la Wanawake wameandaa matukio mbalkimbali ikiwemo ziara ya kwenda kupeleka msaada huo kwa wafungwa wanawake wa mkoa wa Lindi.

Alisema, waliona wasaidie serikali kwa kupeleka msaada huo kwa wafungwa wa kike ambao mara nyingi huwa wanasahaulika sisi tukiwa ni Jukwaa la wazalendo huru tumeona tupeleke msaada huo gerezani.

Katibu wa Jumuhiya ya Wananwake wa jukwaa hilo la Wazalendo Huru Hawa Mcheka alisema kusaidia wenye mahitaji nchini ni moja ya malengo ya jukwaa hilo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali nchini.

Mikel Arteta amkingia kifua Ramsdale
Prof. Mdoe: Tanzania inatambua mchango wa China kiuchumi