Bondia wa ngumi za kulipwa, Hassan Mwakinyo anatarajiwa kupanda ulingoni kutetea ubingwa wake wa WBO, Aprili 27, mwaka huu dhidi ya Rasheed Adeyemo kutoka Nigeria.

Akizungumzia pambano hilo, Mwakinyo amesema pambano hilo la raundi 12 la uzito wa kati, litafanyika Masaki jijini Dar es salaam.

“Sina shaka na uongozi wangu, kwani nina walimu wazuri, nina imani kwa uwezo wa Mungu nitampiga mpinzani wangu. Na kufika hatua nzuri duniani,” amesema.

Mwakinyo aliongeza kuwa kujituma kwake na kupatiwa mazoezi imara ana imani atafanya vyema katika mapambano yake.

“Mashabiki na Watanzania wategemee mambo mazuri kutoka kwangu, kwa sababu mimi na uongozi wangu tunafanya mazoezi yenye viwango vikubwa kuhakikisha tunatoa burudani nzuri ulingoni,” amesema

Mwakinyo atapanda ulingoni akiwa na kumbukumbu kushinda kwa TKO, baada ya kumpiga bondia, Elvis Ahorgah kutoka Ghana, pambano lililofanyika Januari 27, mwaka huu Visiwani Zanzibar.

Diego Simione: Sikuangalia mikwaju ya penati
Klopp akanusha kubaki Liverpool