Mkurugenzi wa Michezo wa Fluminense, Fred, amekiri Thiago Silva bado ni sehemu ya ndoto ya kusajiliwa na klabu hiyo, na wanatumani kumwona akirejea Brazil wakati mkataba wake na Chelsea utakapomalizika.

Miamba hao wa Brazil wameweka wazi nia yao ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye mkataba wake pale Stamford Bridge unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Inaelezwa kuwa beki huyo wa kati amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na klabu hiyo na huzungumza na rais kila wiki.

Anaweza kurejea katika klabu yake ya nyumbani, ambako alicheza kwa misimu miwili na nusu kati ya 2006 na 2009.

Akizungumza na ESPN Brasil, Fred alisema: “Thiago Silva imekuwa ndoto yetu kwa muda mrefu, rais huzungumza naye karibu kila wiki.

“Thiago ana mkataba kule England, tunamlenga, mimi binafsi ni rafiki yangu, ni shabiki mkubwa wa tabia yake, anastahili kila la kheri, anajua hapa milango iko wazi kwake kurudi.

“Tunapaswa kuwa makini ili tusimpe presha Thiago. Mashabiki wanampenda Thiago, tunampenda Thiago na Thiago anaipenda Fluminense. Siku moja ni jambo lisiloepukika, litatokea, ni matakwa ya wachezaji, matakwa ya klabu na tunatumani itatokea hivi karibuni.”

The Blues wanaonekana kutafuta mabeki wa kati kabla ya dirisha la usajili la majira ya joto.

Leny Yoro wa Lille bado anavutiwa na Stamford Bridge, ingawa ripoti zinadai PSG na Real Madrid pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18.

Polisi yatoa tahadhari urafiki wa Mtandaoni
Taharuki Kilosa: Ulinzi na usalama wafika eneo la tukio