Kocha Mkuu wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso anatarajiwa kupendelea kuhamia Bayern Munich ikiwa ataamua kuondoka katika timu yake ya sasa msimu unaokuja wa majira ya joto, ripoti imedai.
Alonso amefurahia msimu mzuri akiwa na Bayern Leverkusen ambao umewaacha kwenye kilele cha kushinda Bundesliga, na uchezaji wa kikosi chake umevutia bila ya kushangaza baadhi ya wababe wa Ulaya, ambao wengi wao wanatafuta makocha wapya kabla ya msimu wa 2024/25.
Miongoni mwa wanaowania saini ya Alonso ni Bayern na Liverpool, wote waajiri wa zamani wa raia huyo wa Hispania wakati wa enzi zake za kucheza, lakini Florian Plettenberg wa Sky Germany anaamini Alonso atajiunga na Bayern ikiwa ataamua kuondoka msimu huu wa majira ya joto.
Wakati kuondoka kwa Alonso kutoka Leverkusen kwa sasa ni mbali na uhakika, inasemekana kwamba kocha huyo angechagua kujiunga na Bayern mbele ya Liverpool ikiwa ataamua kubadili klabu katika miezi ijayo.
Mazungumzo rasmi bado hayajafanyika, lakini maofisa wa Bayern wanaamini Alonso ameamua na angependelea kuhamia Munich.
Mkataba wa Alonso na Leverkusen utaendelea hadi 2026, lakini nahodha wa klabu hiyo, Lukas Hradecky hivi majuzi alikiri kwamba hakuna mtu kwenye chumba cha kubadilishia nguo ambaye atamlaumu bosi huyo ikiwa atachagua kuchukua hatua nyingine katika maisha yake ya soka msimu huu wa majira ya joto.
“Hayo ni matakwa na ndoto yetu yeye kubaki, lakini hakuna atakayekasirika au kubishana ikiwa atashinda Bundesliga na kuamua kwenda kwingine,” alisema Hradecky.