Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha amesema anajua ukubwa wa mchezo ulio mbele yake na kuwataka wachezaji wake kutoihofia Al Ahly ya Misri, pia akiwataka wachezaji wake kupumzisha akili zao ili kupunguza presha ya mechi.

Simba SC itakuwa na kibarua kigumu Ijumaa (Machi 29) itakapotupa karata yake ya kwanza kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Akizungumza kisiwani Unguja, Zanzibar Kocha Benchikha amesema ni mechi muhimu sana wanatambua ubora wa Al Ahly, lakini wachezaji wake hawatakiwi kuhofia zaidi ya kujiweka na kuufikiria mchezo jinsi ya kwenda kupambana na kutafuta ushindi siku ya ljumaa (Machi 29).

Xabi Alonso afumbua fumbo zito

“Tunahitaji kufanya mazoezi mara mbili kwa siku, asubuhi na usiku, lakini pia wachezaji kupata muda wa kupumzika na akili yao kujielekeza zaidi katika mchezo dhidi ya Al Ahly.

“Tunafahamu ubora wa Al Ahly na tumecheza nao mara kadhaa na mara ya mwisho tulioneshana ushindani na ninaamii wanapotuliza akili na kupanbana zaidi kwa kufuata maelekezo tutafanikiwa kuupata ushindi” amesema

Amesema kulingana na programu zake kuelekea mchezo huo, kambi ya Zarzibar inawasaidia hasa kwa wachezaji wake kulingana na mazingira ya kufanyia kazi na kuwataka kusahau yote na kutambua umuhimu wa mhezo dhidi ya Al Ahly.

Katika hatua yingine Benchikha amesema anafurahia kurejea salama kwa baadhi ya wachezaji wake waliokuwa kwenye vikosi vya timu za taifa.

Kisu kikali kwa Liverpool, Arsenal
Xabi Alonso afumbua fumbo zito