Serikali Nchini, imesema itaendelea kuhakikisha inawezesha mazingira bora na rafiki kwa Vijana wabunifu kwa kutoa mikopo, ajira na kuwapa fursa mbalimbali kwa kutumia taaluma vyema katika kung’amua fursa katika jamii.

Hayo yamezungumzwa katika Siku ya Mzumbe na Kambi ya Ujasiriamali, na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli, kwa hadhira iliyohudhuria tukio hilo Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. William Mwegoha wakipata maelezo kutoka kwa wajasiriamali walioshiriki katika Siku ya Mzumbe na Kambi ya Ujasiriamali mwishoni mwa wiki.

Amesema kuna dhana kuwa wasomi wengi wanahisi Serikali haiwasaidii  kupata ajira lakini si kweli na kuwataka wasomi kutumia taaluma zao kubuni  bunifu mbalimbali, kuendana na soko la ajira na kubadilisha mtazamo uliopo wa  kusubiri ajira za Serikali kwani nguvu, fikra  na mtazamo wa kujiajiri ndio unahitajika.

Nguli ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kuhakikisha inawezesha mazingira bora na rafiki kwa vijana wabunifu kwa kutoa mikopo, ajira na kuwapa fursa mbalimbali kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku akiwataka vijana kutumia taaluma vyema katika kung’amua fursa katika jamii.

Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu, Prof. Eliza Mwakasangula akipokea Tuzo ya mshindi bora katika Machapisho ya Kitaaluma.

“Leo limefanyika tukio kubwa katika historia, sisi kama Serikali nichukue nafasi hii kuwahidi wasomi kuwa watapata ushirikiano wa kutosha, tunafursa nyingi Serikalini, niseme dunia imebadilika, mazingira yamebadilika, tunafundishwa ili taaluma zetu tukazitumie katika maisha ya kawaida, nawaomba sana vijana tuwaze nje ya box kwa kuwa na mawazo ya ubunifu  na sisi kama Serikali tutaunga mkono mawazo hayo,” amesema Nguli.

Xabi Alonso afumbua fumbo zito
Kipato cha Mwanamke: Mradi mazao ya uvuvi wazinduliwa