Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa kundi la wazazi, MNEC. Hamoud Jumaa amewataka Viongozi wa kuchaguliwa kunadi miradi ya maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya CCM katika maeneo yao, badala ya kujinadi wenyewe.

Jumaa ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Kibaha na kudai kuwa Rais Samia amekuwa akitoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo baadhi yake tayari imekamilika na Wananchi wameanza kupata huduma.

Amesema, “kuna baadhi ya Viongozi, Wabunge tunapita huko sehemu mbalimbali hatusikii wakisema wanasema nimefanya mimi, pikipiki zile nimeleta mimi, mitungi ya gasi nimeleta mimi gari nimeleta mimi, shule nimeleta mimi.”

Jumaa ameongeza kuwa Viongozi hao pia husema, “barabara nimeleta mimi wakati mheshimiwa rais katika hotuba zake anasema nimejenga shule zaidi ya 500, barabara kila wilaya na kila jimbo na kila halmashauri pia ametoa bilioni nyingi za kujenga barabara za halmashauri hizo.”

Mradi uendelezaji wa Bonde la Msimbazi waiva
Mmoja asombwa na maji, Nyumba 100 zabomolewa Kilombero