Baraza la Sanaa la Taifa – BASATA, limesitisha rasmi shughuli za Sanaa, sherehe na burudani katika kumbi 504 za Tanzania Bara ambazo hazikutimiza agizo la uhuishaji wa vibali vyao.
Taarifa ya iliyotolewa kwa umma na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Kedmon Mapana imeeleza kuwa, Februari 19, 2024 BASATA Ilitoa tamko la nia ya kusitisha huduma kwa kumbi 653 ndani ya siku 14 kwa wadau wote ambao hawatatimiza vigezo vya kuhuisha vibali vya kufanya shughuli za Sanaa, Sherehe na Burudani nchini.
Amesema, ni Kumbi 149 pekee zilizotekeleza agizo hilo na hivyo kupitia masharti ya usajili ya Kanuni ya 59 likasitisha shughuli hizo kuanzia Machi 28, 2024 mpaka watakapolipia vibali kupitia kiungo https://sanaa.go.tz. kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za Serikali wakiwemo Maafisa Utamaduni.
Amesema, Ofisi za BASATA zitakuwa wazi kwa siku ya Jumamosi na Sikukuu kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa sita mchana kwa ajili ya kutoa huduma, huku likikumbusha Wamiliki wa kumbi ambao hawajasajiliwa/hawanavibali hai vya kuendesha shughuli za Sanaa, starehe na burudani kujisajili mara moja ili kuepuka usumbufu.
ANGALIA ORODHA YA KUMBI ZILIZOSITISHIWA HUDUMA.