Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametuma salam za pole kwa familia za watu 45 waliofariki katika ajali ya basi ambalo lilikuwa na abiria 46, lililotumbukia kwenye korongo umbali wa mita 50 kutoka kwenye daraja, huku Msichana (8), ndiye pekee aliyenusurika.

Basi hilo lilianguka kwenye kizuizi na kuwaka moto lilipogonga kingo ya ardhi katika mkoa wa kaskazini-mashariki mwa Limpopo, likiwa na Mahujaji waliokuwa wakisafiri kutoka mji mkuu wa Botswana Gaborone kwenda katika Tamasha la Pasaka katika mji wa Moria.

Gari hilo linadaiwa kupoteza mwelekeo na katika njia ya mlima ya Mmamatlakala kati ya Mokopane na Marken, karibu kilomita 300 (maili 190) kaskazini mwa Johannesburg, ambapo Waziri wa Uchukuzi, Sindisiwe Chikunga alitoa rambirambi kwa familia zilizoathiriwa na ajali hiyo.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 30, 2024
BASATA yasitisha shughuli za Kumbi 504