Ama kweli Dunia ina mambo mengi ya kushangaza. Hebu mtazame huyo jamaa Pichani hapo chini.

Anaitwa Max More, yeye ni Bilionea Raia wa Kampuni ya Alcor Life Extension inayopatikana Jimbo la Arizona Nchini Marekani, ambayo ilianzisha mradi wa kuhifadhi miili ya watu waliofariki kwa kuiweka kwenye baridi kali ndani ya friji, wakitaraji kuja kuwafufua wafu hao ifikapo mwaka 2040 kwa kutumia teknolojia ambayo wamedai bado wanaifanyia utafiti.

Kampuni hiyo inamilikiwa na Bilionea Max More ambaye anasema alitumia miaka 12 kufanya kazi katika Wakfu wa Kampuni kongwe zaidi ya uchapishaji duniani, kwanza kama Mkurugenzi Mtendaji na kisha kama balozi na rais aliyestaafu, kabla ya kuachia ngazi na kuanzisha mradi wake huo ambao umeibua maswali mengi ya kisayansi, kisheria, kimaadili na kifalsafa.

Dkt. Jerry Lemler, Rais wa zamani na Mkurugenzi Mtendaji wa Alcor Life Extension Foundation, akiwa amesimama katika eneo la Patient Care Bay ambapo miili ya watu 49 vimehifadhiwa katika baridi, katika Makao Makuu ya Kampuni huko Scottsdale, Arizona, Julai 12. 2002. Picha ya Jeff Topping/Reuters.

Alcor imedai kuwa tayari ina miili 224 iliyohifadhiwa katika kituo chake cha hali ya juu huko Scottsdale, Arizona na ikiwa na Wanachama hai 1,418 waliojiandikisha kwa hiari yao na kusaini mikataba ya kuja kuhifadhiwa kituoni hapo baada ya kufa na kufufuliwa kipindi ambacho Teknolojia hiyo itakapoanza kufanya kazi.

Madai ya kuanzisha mradi huo, yaliibuka baada ya wenye Kampuni kudai Vitabu vya dini vinaelekeza kwamba mtu akifa, basi baadaye atakuja kufufuliwa na hivyo wao kama Alcor Life Extension wamegundua utaalamu huo na wataanza kuutumia utaalamu huo mwaka 2040 kwani kwasasa hakuna njia ya kufufua watu.

Gari maalum kwa ajili ya kusafirisha miili itakayohifadhiwa ambayo ilioneshwa kwenye mkutano huko Madrid Novemba 2022. Picha ya Ricardo Rubio/Europa Press.

Hata hivyo, dai hili limekatakiwa na Prof. Arthur Caplan wa bioethics katika Chuo Kikuu cha New York cha Grossman School of Medicine, akisema ni jambo lisilowezekana na hakuna mtu ataweza kufanya hivyo hata miaka 1,000 ijayo, madai yanayopingwa na baadhi ya watu wakisema miaka 100 iliyopita pia, watu hawakuamini kama inawezekana kutua juu ya mwezi.

Hata hivyo, mtu mmoja alihoji akidai itakuwaje aliyekufa atakaporudi kuwa hai, akitolea mfano wa Malkia Elizabeth II angehifadhiwa kwa akafufuka je? angekuwa mfalme tena. Je? watu wangekuwa na madai ya bidhaa na mali zao ambazo zilirithishwa kwa wengine, pia akasema ni vigumu watu waamke mamia kwa maelfu kisha kwaje kujumuika katika ulimwengu mpya ambao hawaelewi.

Seti za kushangaza za kisayansi zilizowahi kuoneshwa katika kipindi cha televisheni cha ABC ‘The Wide World of Mystery’, kipindi cha ‘The Two Deaths of Sean Doolittle’. Picha ya American Broadcasting Companies/ Getty Images.

BASATA yasitisha shughuli za Kumbi 504
Amnesty yalia na ukiukwaji haki za Binadamu