Maafisa nchini Peru wamevamia nyumba ya Rais Dina Boluarte siku ya Jumamosi kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea wa ufisadi unaohusiana na saa za kifahari za Rolex ambazo hakuzitaja, hatua iliyolaaniwa vikali na serikali.

Takriban maafisa 40 walihusika katika uvamizi huo, ambao ulikuwa unatafuta saa za kifahari aina ya Rolex ambazo Boluarte hakuwa amezitangaza hadharani. Polisi imesmea uvamizi huo ulikuwa wa kufanya upekuzi na kukamata.

Rais huyo anaekabiliwa na misukosuko hakuwepo Nyumbani huku Waziri Mkuu Gustavo Adrianzen alilaani uvamizi huo kwa kusema, “hii ni ghadhabu isiyovumilika na iliovuka mipaka na ni kinyume cha katiba.”

Maafisa walianzisha uchunguzi dhidi ya Boluarte mwezi huu baada ya chombo cha habari kuangazia picha za saa zake za kifahari za michezo kwenye hafla za umma na uvamizi huo, ulikuwa operesheni ya pamoja kati ya polisi na ofisi ya mwendesha mashtaka.

Aomba msaada kwa Rais Samia, DC atoa neno
Walaani tukio kushambuliwa kwa Ole Sendeka