Tukio la unajimu liko tayari kuwavutia watazamaji wa anga likifahamika kwa umaarufu kwa jina la kupatwa kwa jua, ambapo inawezekana kabisa mchana ukawa usiku kwa baadhi ya maeneo hii leo Aprili 8, 2024.
Kupatwa kwa jua ni jambo la kiastronomia ambapo Mwezi huwa kati ya Dunia na Jua na kuziba nuru ya Jua kabisa au kwa kiasi. Mwezi unafunika jua kabisa, hutoa kivuli duniani na kutengeneza kile kinachoitwa “njia ya jumla.”
Watu wanaweza kushuhudia kupatwa kwa jua endapo hali ya hewa itakuwa ya kuridhisha kutegemeana na mpangilio na kutokana na uso wa dunia kwani kunaweza kubadilika hali kulingana na majira ya mwaka.
Hali hii itaonekana katika umbali wa kilomita 185 kati ya Mexico, Marekani na Canada na pia Mataifa mengine 18 pia yatafanikiwa kupata kuiona hali hiyo, isipokuwa nchini India.
Tukio hili litachukua muda wa takriban saa mbili na nusu, lakini kiujumla litadumu kwa dakika 4 na sekunde 27 kwenye njia ya giza kuu, huku Watazamaji wa anga kote ulimwenguni wakishauriwa kuvaa vitu vya kujikinga, kama vile miwani iliyoidhinishwa ya kupatwa kwa jua, kwani kukosa kufanya hivyo kunaweza kuchoma retina ya jicho lako na kusababisha uharibifu wa kudumu au hata upofu.