Mwenge wa Uhuru Mwaka 2024 umepokelewa Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro, baada ya kumaliza mbio zake kwenye Wilaya ya Mwanga ambapo makabidhiano yamefanyika viwanja vya Shule ya Msingi Njoro, Halmashauri ya Wilaya ya Same.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amepokea mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Abdallah Mwaipaya akisema ukiwa wilayani humo utakimbizwa umbali wa km138.4 ambapo utatembelea, kuweka Mawe ya Msingi na kuzindua jumla yamiradi Nane yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.6.

Wilaya ya Same inakua Wilaya ya Saba kwenye Mkoa wa Kilimanjaro na ndio itahitimisha mbio hizo Kimkoa kwa mwaka huu wa 2024, kisha kukabidhiwa Mkoa jirani wa Tanga hapo kesho Aprili 9, 2024.

Coastal Unoin yakanusha kumtega Ouma
MALIMWENGU: Tukio kubwa la unajibu Aprili 8, 2024