Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris St-Germain wamepaga kulipa Pauni 111.5 milioni kumnunua Mshambuliaji wa SSC Napoli, Victor Osimhen katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Staa huyo wa kimataifa wa Nigeria kwenye mkataba wake kuna kipengele ambacho kinamruhusu kuondoka ikiwa timu inayomtaka italipa kiasi hicho cha pesa.

PSG imekuwa ikimuwinda nyota huyo tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi, ili awe mbadala wa mshambuliaji Kylian Mbappe ambaye ataondoka mwisho wa msimu huu.

Osimhen alivivutia vigogo vingi barani Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu msimu uliopita ambapo alikuwa mfungaji bora wa Serie A akiwa na mabao 26.

Katika msimu huu licha ya SSC Napoli kutofanya vizuri, Osimhen ameendelea kufanya vizuri ambapo amefunga mabao 13 kwenye mechi 25 za michuano yote.

Chelsea na baadhi ya timu za Saudi Arabia pia zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili staa huyo.

MALIMWENGU: Tukio kubwa la unajibu Aprili 8, 2024
Che Malone atikisa kibiriti Simba SC