Johansen Buberwa – Kagera.
Watanzania wameaswa kuacha tabia ya mizozo na migogoro jambo ambalo linapelekea kurudisha maendeleo nyuma na baadhi ya watu kupata laana na kuwa dhaifu kitu ambacho ni kinyume na mapenzi ya Mungu.
Akizungumza wakati wa Iftar iliyo andaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera iliyohusisha viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini,siasa na taasisi
Kingozi wa Tasisi ya Kiislamu Kanda ya Ziwa, Sheikh Abdul Shahidu amesema jamii imesahau amri za Mungu na suala la migogoro limetangulizwa mbele.
Amesema, Watanzania wanatakiwa kuendelea kulinda tunu muhimu kwenye Taifa ambayo ni amani ilikuweza kujiletea jmaendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kiujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajath Fatma Mwasa amewataka Wazazi na walezi wa Mkoa humo kuweka nguvu kubwa kwa watoto wao, ili wapate fursa zinazopatikana ndani ya Mkoa huo.