Lydia Mollel – Mvomero – Morogoro.

Mamlaka ya Usimamizi Wanyama Pori Nchini – TAWA imefanikiwa kumuua Mamba anayedaiwa kuwajeruhi Wananchi kadhaa wa Kitongoji cha Gudugudu kilichopo kijiji cha Mlali Wilayani Mvomero, Mkoani Morogoro .

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Judith Nguli, Wananchi hao wamesema Mamba hao wameanza kuonekana katika kipindi hiki ambacho Mvua zinaendelea kunyesha, hasa katika mto Mlali ambao unapita pembezoni mwa kijiji hicho.

Wamesema, idadi kubwa ya Mamba iliwafanya Wananchi waliamua kuacha kujiusisha na shughuli za Kilimo kwenye mashamba yote ambayo mto Mlali unapitisha maji yake Jambo ambalo linaweza kusababisha wanachi kukosa chakula na kusababisha Kuwepo kwa baa la njaa.

Kufuatia changamoto hiyo, Serikali kupitia TAWA imeweka kambi kwenye kijiji hicho ili kuwatafuta Mamba ambao wamekuwa wakisababisha madhara kwa wananchi, huku Mhifadhi kutoka TAWA, Gilbert Magafu akiwataka Wananchi kuchukua tafadhari kwani mito yote inayopita kijiji hapo imejaa maji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Judith Nguli amesema baada ya kuwepo kwa taarifa za uwepo mamba kwenye kijiji hicho hasa katika mto Mlali, Serikali iliagiza wauliwe ili wasilete madhara kwa Wananchi.

Sheikh Shahidu: Migogoro haileti maendeleo, ni laana
Cancelo akataa kurudi England