Joao Cancelo amedhamiria kupata uhamisho wa kudumu Barcelona wakati wa majira ya joto licha ya Chelsea, Arsenal na Bayern Munich kumuwindwa.

Beki huyo wa pembeni alijiunga na Barca kwa mkopo siku ya mwisho ya uhamisho wa majira ya joto, amekuwa mchezaji muhimu kwa klabu hiyo tangu wakati huo.

Cancelo ameichezea ‘La Blaugrana’ mara 32, na hivyo kuimarisha nafasi yake kama chaguo la kwanza la beki wa kushoto chini ya Xavi Hernandez.

Kwa mujibu wa Sport, Cancelo anataka kubaki klabuni hapo mara baada ya mkopo wake wa sasa kuisha, huku wakala wake Jorge Mendes kwa sasa akijaribu kusaidia kuwezesha mazungumzo kati ya klabu yake mama ya Man City na wababe hao wa La Liga ili kufanikisha hilo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa City wamekuwa wakitaka kupata pauni milioni 40 kwa ajili ya huduma ya mchezaji huyo, huku Arsenal, Chelsea na Bayern Munich wakiwa miongoni mwa klabu nyingine zinazomuwania.

Inasemekana Barca walimwambia Cancelo kuhusu nia yao ya kutaka kumbakisha, jambo ambalo beki huyo wa pembeni alitarajia kulikubali.

Licha ya ofa anazoweza kupokea kutoka kwingineko msimu huu wa majira ya joto, Cancelo anabakia kuridhika na Barcelona na yuko imara katika nia yake ya kuendelea kucheza La Liga.

Chaguo zinazozingatiwa kuongeza muda wa kukaa kwa Cancelo huko Katalunya ni pamoja na uhamisho wakati wa dirisha lijalo la majira ya joto, au mpango wa mkopo wenye chaguo la ununuzi linalofuata.

Juhudi zinaendelea ili kuangazia vikwazo vya mishahara ya Barca, lakini dalili zinaonesha kuwa mpango huo unaweza kukamilika kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro.

Mamba wazua kizaazaa Mlali, TAWA waokoa jahazi
Oparesheni maalum Mvomero: Wananchi kutoa ushirikiano