Lydia Mollel, Mvomero – Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli amepokea timu ya Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi – JWTZ, kwa ajili ya kuchunguza na kisha kulipua vyuma vinavyotajwa kuwa ni mabomu katika Wilaya hiyo, ambavyo vimekuwa vikiokotwa na Wananchi katika maeneo mbalimbali.

Kutokana na ugeni huo, DC Nguli amewaomba Wananchi wote katika wilaya ya Mvomero kutoa ushirikiano kwa maafisa hao, ili waweze kutimiza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuokota vyuma vyote vinavyotajwa kuwa ni Mabomu ili visilete madhara.

Cancelo akataa kurudi England
V8 jingine ladakwa na Wahamiaji haramu Mafinga