Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) unatarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu katika mkoa utakaotangazwa baadaye, imeelezwa.

Kwa mujibu wa kalenda ya matukio ya mwaka, RT watafanya uchaguzi wao kupata Rais, Makamu wa Rais na wajumbe wengine watakaoongoza kwa miaka minne ijayo.

Uchaguzi huo utatanguliwa na mkutano mkuu ambao taarifa mbalimbali zitasomwa zikiwemo zile za ukaguzi wa fedha, taarifa ya katibu mkuu na zingine ili kujua maendeleo ya miaka minne ya riadha.

Agosti na Septemba kitakuwa kipindi cha kufanyika kwa uchaguzi wa mikoa ambapo viongozi watakaochaguliwa ndio watapiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa RT utakaofanyika Desemba.

Juni 8 hadi 12 kutakuwa na mashindano ya wakubwa ya riadha ya Afrika yatakayofanyika Cameroon huku Julai kutakuwa na Dodoma Marathoni itakayofanyika Dodoma.

Michezo ya Afrika ya Majeshi itafanyika Novemba nchini Nigeria na nchi mbalimbali za Afrika zitashiriki kabla ya Mashindano ya Dunia ya Majeshi au Cisim.

Juni kutakuwa na Michezo ya Shule za Msingi na Sekondari (Umitashumta na Umisseta) yatakayofanyika mkoani Tabora.

Arteta: Nimeshasahau ya msimu uliopita
Sheikh Shahidu: Migogoro haileti maendeleo, ni laana