Kocha Mikel Arteta amedai kuwa amesahau kuhusu mwisho wa kusikitisha wa Arsenal kwa kampeni ya Ligi Kuu ya 2022/23 ambapo walimaliza kwa pointi tano nyuma ya mabingwa, Manchester City.

Arsenal walibwaga mbio za ubingwa wa taji la Ligi Kuu msimu uliopita mbele ya Man City walioshinda mataji matatu, licha ya kwamba Washika Bunduki hao kuna wakati walikuwa kileleni mwa jedwali kwa tofauti ya pointi nane.

Kocha wa Arsenal, Arteta anaamnini kuwa msimu uliopita ni habari ya zamani, na anadai kuwa ameifuta akilini mwake.

Arteta aliulizwa kuhusu tofauti kati ya mwaka huu na uliopita na alisema: “Nadhani tuko katika wakati mzuri sana. Tuna kikosi kikiwa na afya njema na nguvu nzuri na kujiamini sana binafsi na kwa pamoja. Tunapaswa kuendelea tu kufanya kile tunachofanya.

“Kai Havertz hakika ana mchango mkubwa kwenye timu. Uchezaji wake kwa ujumla umekuwa mzuri sana na sasa idadi yake ya uchangiaji wa mabao iko juu sana. Anahitaji kudumisha hilo.

“Nadhani uelewa wake na wachezaji wa kushambulia ulikuwa mzuri sana. Nadhani walikuwa na lengo la kweli na muunganisho na uwazi mwingi wa wapi pakushambulia na tulitengeneza nafasi nyingi.”

Alipoulizwa kuhusu msimu uliopita, maneno ya Arteta yalikuwa: “Nimesahau tayari.

Arsenal wanatumaini kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20. Pia wapo kwenye Ligi ya Mabingwa na watamenyana na Bayern Munich katika mkondo wa kwanza wa Robo Fainali baadae leo Jumanne (Aprili 09).

TCB kuadhimisha miaka 100 ifikapo 2025
Riadha kuchaguana Desemba 2024