Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye (48), amemuagiza Waziri wake Mkuu, Osmane Sonko kuandaa mpango wa dharura wa kuimarisha uchumi na sekta ya fedha.
Faye alipata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa mwezi uliopita kwa ahadi ya mageuzi makubwa na kuwa rais mwenye umri mdogo zaidi licha ya kuwa hakuwahi kushikilia wadhifa wa kuchaguliwa.
Alimuagiza Sonko kufanya tathmini ya jumla ya programu na mipango na kutoa ripoti kuhusu hali ya jumla ya fedha za umma, ushirikiano wa kimataifa na wa sekta ya umma na binafsi.
Taarifa ya agizo hilo ilitolewa baada ya kikao chake cha kwanza na Baraza la Mawaziri, Faye akimpa Sonko hadi mwisho wa mwezi huu (April), kutamatisha mpango huo na kuhakikisha utekelezwaji wake.