Lydia Mollel – Morogoro.

Katika kuhakikisha juhudi za Serikali za kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira nchini zinaungwa mkono, Vijana Mkoani Morogoro wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupata elimu juu ya kujikwamua kiuchumi kwa kujiajiri wenyewe.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Ufaulu Project Tanzania, Simon Joseph ameyaeleza hayo na kusema anatambua hali ya ukosefu wa ajira miongoni mwa Vijana, hivyo wameandaa semina maalum itakayowapa mafunzo na kuwawezesha kujiajiri.

Amesema, “moja ya  ajenda katika semina hiyo ni kutoa elimu ya afya kwa vijana ili waweze kutambua njia sahihi za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi, kuchangia damu kupitia mpango wa Taifa wa Damu Salama, pamoja na kushughulikia masuala ya kisaikolojia na kutoa elimu juu ya ubunifu na kujiongeza kwa vijana.”

Naye Patrick Ndawogo, Mkurugenzi Mtendaji wa UCDP Tanzania amesema lengo lao ni kusaidia vijana kujikwamua kiuchumi na kupata fursa za ajira ndani na nje ya nchi, kama njia mojawapo ya kusaidia Serikali kupunguza tatizo la ajira nchini.”

“Semina hiyo itafanyika tarehe 4 mwezi Mei katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) na imepewa jina la ‘Nje ya Box’ kwa lengo la kuwasaidia vijana kupata maarifa ya kujiongeza na kufikiria zaidi ya maarifa ya darasani, kuwa na uwezo wa kujiajiri, na kutafuta ajira ndani na nje ya nchi pindi watakapohitimu masomo yao,” alisema.

Mwl. Tengwa: Hali ni mbaya, Vijana waambiwe ukweli
Faye amtaka Sonko kuimarisha uchumi, sekta ya fedha